Abigail Chams akosa tuzo ya BET yanyakuliwa staa wa Brazil.
Joyce Shedrack
June 10, 2025
Share :
Msanii wa muziki wa bongofleva Nchini Abigail Chams ameikosa tuzo ya BET kwenye kipengele cha Msanii Mpya wa Kimataifa, baada ya kutangazwa kuwa Ajuliacosta kutoka Brazil ndiye mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka huu.

Abigail aliwasili Los Angeles na mameneja wake Seven Mosha na Gabrielle Chams, akihamasisha mashabiki kupiga kura kupitia likes na comments mitandaoni na alionekana kuongoza mwanzoni lakini ameshindwa kuibuka mshindi wa tuzo hiyo.
Licha ya staa huyo kutofanikiwa kutwaa tuzo hiyo iliyotolewa usiku wa jana huko Los Angeles Marekani lakini heshima ya kutajwa pamoja na mastaa wakubwa ilikuwa ushindi kwa tasnia ya muziki wa Tanzania.