Afariki akifuata 'diety' ya kula matunda tu
Sisti Herman
October 14, 2025
Share :
Karolina Krzyzak mwanamke mwenye umri wa miaka 27 kutoka Poland, alifariki kwa uchovu mkubwa huko Bali baada ya kufuata lishe kali ya matunda pekee. Inaripotiwa kuwa alikataa kula chakula chochote kilichopikwa au kilichosindikwa na pia alikataa matibabu ya hospitali.
Wakati wa kifo chake, Karolina alikuwa na uzito wa chini ya paundi 50 takriban kilo 22, mwili wake ukiwa umeishiwa nguvu kutokana na miaka ya ulaji wa kujinyima kupita kiasi.