pmbet

Afungwa jela maisha kwa kumlawiti mtoto wa miaka 14.

Joyce Shedrack

May 7, 2025
Share :

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Lindi imemhukumu Salum Bakari Ally, maarufu kama Maroganya (60), mkazi wa Halmashauri ya Mji wa Mtama, Wilaya ya Lindi, kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 14.

Mtuhumiwa alikamatwa Oktoba 12, 2024 na kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Desemba 30, 2024, ambapo alisomewa shtaka linalomkabili na kukana.

Afungwa maisha kwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la kwanza - SwahiliTimes
Upande wa Jamhuri, ukiongozwa na Wakili Mwandamizi Mofath Sett, uliwasilisha vielelezo viwili mahakamani kama ushahidi wa kuthibitisha kosa hilo.

Akisoma hukumu ya kesi namba 36152/2024, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Bi. Consolatha Singano, alisema mahakama imeridhika pasipo shaka kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo, na hivyo kumhukumu kifungo cha maisha gerezani ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Wakazi wa Mtama wameipongeza mahakama kwa kutoa hukumu hiyo wakisema ni hatua muhimu katika kulinda haki za watoto na kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea kushamiri vijijini.

Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Lindi, Bw. Richard Kimaro amesema hukumu hiyo• inatoa ujumbe mzito kwa jamii na wazazi kuwa makini na ulinzi wa watoto wao. “Tunahitaji ushirikiano wa karibu kati ya wazazi, walimu na vyombo vya dola ili kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya vitendo vya ukatili wa kingono,” alisema.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet