Agather apatikana mpakani mwa Uganda na Tanzania
Sisti Herman
May 23, 2025
Share :
Mwanaharakati wa Uganda, Agather Atuhaire amepatikana leo baada ya kutelekezwa katika mpaka wa Tanzania na Uganda.
Agather Atuhaire pamoja na Boniface Mwangi wa Kenya walikamatwa mara baada tu ya kuwasili nchini Tanzania kufuatilia kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu.