pmbet

Aigiza kufa ili kujua wangapi wangeshiriki msiba wake

Eric Buyanza

October 18, 2025
Share :

Huko nchini India, mzee aliyefahamika kwa jina la Mohan Lal (mwanajeshi mstaafu) mwenye umri wa miaka 74 ambaye alitaka kuangalia ni nani angehuzunika na kifo chake, amethubutu kuigiza kuwa amekufa ili kuona idadi ya wale ambao wangehudhuria msiba wake.

Watu wa kijiji cha Konchi katika jimbo la Bihar walishtushwa kusikia kuhusu kifo cha ghafla cha Mohan ambapo wengi wao walishiriki katika ibada zote za jadi kwa ajili ya kuombea marehemu. 

Hata hivyo wakati wananchi hao wakijiandaa kumpeleka sehemu mbayo maiti huchomwa, ghafla walipatwa na mshtuko kumuona Mohan akiinuka kutoka kwenye jeneza. 

"Nilitaka kushuhudia mwenyewe na kujua ni kiasi gani heshima na upendo watu hunipa," Mohan alisema alipoulizwa kwa nini amefanya kituko hicho.

Mohan aliwatumia ndugu na baadhi ya jamaa zake kumsaidia kueneza habari kuhusu kifo chake na akawaagiza watu wengine wampeleke kwenye mahali pa kuchomea maiti kwenye jeneza lililopambwa ili kufanya tukio hilo liwe na sura ya uhalisia. Mamia ya wakazi wa kijiji hicho walijaa kwenye msiba huo feki jambo ambalo lilimfurahisha sana Mohan.

Ili kuwafanya wenyeji wamsamehe kwa tukio hilo, Mohan Lal aliandaa sherehe kubwa kwa ajili ya wanakijiji hao.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet