Air Tanzania kuanza safari ya Dar, Entebbe na Zanzibar
Sisti Herman
May 16, 2025
Share :
Air Tanzania kuanzisha safari za Dar es Salaam – Entebbe – Zanzibar kuanzia Mei 16, 2025.
Kampuni ya Ndege ya @airtanzania_atcl imetangaza kuanzisha safari mpya zitakazounganisha miji ya Dar es Salaam, Entebbe na Zanzibar kuanzia Mei 16, 2025.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Air Tanzania, safari ya kwanza itaanzia Dar es Salaam hadi Entebbe saa 5:30 asubuhi na kufika saa 7:20 mchana. Baada ya hapo, ndege hiyo itaendelea na safari kutoka Entebbe kwenda Zanzibar kuanzia saa 8:10 mchana hadi saa 10:05 jioni.
Safari ya mwisho itaanzia Zanzibar kuelekea Dar es Salaam saa 10:40 jioni na kutua saa 11:10 jioni.