Al Hilal watonesha kidonda cha wananchi wapamsua TP Mazembe 2-1.
Joyce Shedrack
December 8, 2024
Share :
Klabu ya Al Hilal Omdurman imepata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo wa Kundi A wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa katika dimba la Cheikha Ould Boidiya Nchini Mauritania.
Matokeo ya timu hizo mbili ambazo zipo kundi moja na klabu ya Yanga yanaipeleka Al Hilal nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi hilo baada ya kushinda michezo yote miwili na kukusanya alama 6.
MSIMAMO Kundi A
Al Hilal — mechi 2 — Alama 6
MC Alger — mechi 2 — Alama 4
TP Mazembe — mechi 2 — Alama 1
Yanga Sc — mechi 2 — Alama 0