pmbet

Aliacha kutumia ubini wa Babu kwasababu alikuwa Mvivu

Sisti Herman

May 23, 2025
Share :

Sergio Aguero, nyota wa zamani wa Man City anatupa kisa cha kutotumia jina la baba yake Aguero Del Castillo kwenye utambulisho wake kwenye soka.

 



"Kwa nini jina langu la mwisho ni Agüero na sio Castillo, ambalo ni jina la mwisho la baba yangu? Kwa sababu alikuwa mvivu.

"Ni hadithi ndefu ambayo si watu wengi wanajua. Wazazi wangu wanatoka Tucumán, na wakati huo ilibidi uwe na umri wa zaidi ya miaka 21 ili kusajili mtoto kwa jina lako (mzazi wa kiume) la mwisho.

“Baba yangu alikuwa na umri wa miaka 18 na alitamani kucheza soka. Mama yangu alipopata ujauzito baba yangu alikuwa na umri mdogo. Hakukuwa na mtu mzima wa kwenda naye kujaza taarifa zangu za jina la mwisho … kwa hiyo hospitalini walisema, ‘Itatubidi kumpa jina la mwisho la mama.’ Na hivyo ndivyo nilivyoishia kuwa Sergio Agüero.

"(Baba) Alipofikisha umri wa miaka 21 hakuniandikisha kwa jina lake. Kwa sababu alikuwa mvivu. Baadaye, nilipokuwa na umri wa miaka 18 au 19, nilipokuwa Hispania, aliniambia anataka kubadilisha jina langu la mwisho. Lakini wakati huo nilikuwa tayari natumia Kun Agüero, kila mtu alinijua kwa njia hiyo. Nilimwambia, 'Hapana, wewe ni mjinga. Siwezi kubadili chochote kwa sasa. Sasa sikutambui kama baba yangu'.

“Lakini nilirudi Argentina na kubadilisha taarifa zangu upya, hati za kusafiria na karatasi zingine nikabadili jina na kuweka moja tu la Aguero (jina la kwanza la baba yake) na nilimwambia hilo moja inatosha."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet