Aliyehusishwa kutua Yanga atimkia Al Ahly Misri.
Joyce Shedrack
May 13, 2025
Share :
Kocha Mkuu wa Orlando Pirates raia wa Hispania Jose Riveiro anatajia kujiunga na klabu ya Al Ahly kumrithi kocha Marcel Koller aliyetimuliwa baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Mamelodi Sundowns.

Riveiro atajiunga rasmi na klabu hiyo hivi karibuni na atakiongoza kikosi cha Al Ahly kwenye Kombe la Dunia ngazi ya klabu mwezi ujao Nchini Marekani.
Katika misimu yake mitatu akiwa Pirates, Riveiro ameshinda makombe matano ya nyumbani na kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi kwa misimu miwili mfululizo, kati ya mataji matatu aliyoshinda ni mataji matatu mfululizo ya MTN8 na mawili ya Nedbank Cup.
Kocha huyo siku ya leo ataagwa rasmi ndani ya klabu ya Orlando akiiongoza katika mchezo wake wa mwisho kukinoa kikosi hicho katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Golden Arrows.