pmbet

Aliyeua wafanyakazi wawili wa ubalozi wa Israel ashitakiwa kwa mauaji

Eric Buyanza

May 23, 2025
Share :

Mtuhumiwa pekee wa mauaji ya wafanyakazi wawili wa ubalozi wa Israel mjini Washington Elias Rodriguez amefunguliwa mashtaka Alhamisi katika mahakama ya shirikisho kwa makosa mawili ya mauaji. 

Rodriguez, mzaliwa wa Chicago anatuhumiwa kwa kuwafyatulia risasi watu walipokuwa wakiondoka kwenye hafla iliyowakutanisha wataalamu chipukizi na wanadiplomasia, iliyoandaliwa na Kundi la Wayahudi linalopambana na chuki dhidi yao.

Kulingana na nyaraka za mashitaka, Rodriguez aliwaambia polisi kwenye eneo la tukio kwamba alifanya hivyo kwa ajili ya Wapalestina na Gaza.

Waliouawa kwenye tukio hilo la Jumatano usiku ni Yaron Lischinsky na Sarah Lynn Milgrim, ambao walikuwa mbioni kufunga ndoa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet