Aliyewafanya wahamie Hispania ataendelea kuinoa Uingereza.
Joyce Shedrack
July 16, 2026
Share :
Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) limefikia uamuzi wa kuendelea na Thomas Tuchel kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya hadi michuano ya EURO 2028.
Uamuzi huo unaungwa mkono na pande zote mbili, huku Tuchel pia akithibitisha kuwa ataendelea na majukumu yake kwa mujibu wa mkataba wake unaomalizika mwezi Julai 2028.
"Nitaendelea kubaki na kuiongoza Uingereza Nina mkataba hadi Julai 2028, ingawa kwa sasa ni vigumu kufikiria kuhusu muda huo kutokana na hali ilivyo."
Licha ya changamoto na maumivu ya matokeo ya usiku wa jana dhidi ya Argentina Uingereza bado ina imani na uwezo wa kocha huyo Mjerumani kuijenga timu na kuiongoza kuelekea mafanikio katika michuano ijayo ya Ulaya mwaka 2028.





