Ananzo asepa na Milioni 12 za Davido kisa Challenge ya ngoma yake.
Joyce Shedrack
May 6, 2025
Share :
Staa wa Afrobeat kutoka Nigeria David Adeleke maarufu Davido amemzawadia shabiki yake dola 5000 ambazo ni sawa na Milioni 12 za Kitanzania baada ya kucheza wimbo wake vizuri 'With You' aliomshirikisha Omah Lay kutoka kwenye albamu yake ya 5ive.
Shabiki huyo anayejulikana kama Ananzo ambaye ni mtumiaji maarufu wa mtandao TikTok kutoka Ghana alimbariki Davido baada ya kufanya challenge ya wimbo huo kikamilifu na kufanikiwa kuondoka na Milioni 12 za msanii huyo.
Albamu ya 5ive yenye nyimbo 17 ikiwemo 'With You' aliyomshirikisha Omah Lay ilitoka Aprili 18, 2025 na kuwa albamu ya tano kutoka kwa Davido imekuwa na mafanikio makubwa tangu kuachiwa kwake huku ikiongoza kwa wasikilizaji wengi kupitia majukwa mbalimbali ya kidijitali.