pmbet

Antonov An-124 bado haijapata mpinzani wa kubeba mizigo duniani

Eric Buyanza

August 8, 2025
Share :

Antonov An-124, iliyotengenezwa na Ofisi ya Usanifu ya Antonov ya Ukraine wakati wa enzi ya Usovieti, inasalia kuwa ndege kubwa zaidi ya kijeshi ya usafirishaji duniani kwa uwezo wa kubeba mizigo. 

Ilianzishwa 1986, inatumiwa na Jeshi la Anga la Urusi na Mashirika ya Ndege ya Volga-Dnepr kwa misheni za kibiashara na kijeshi katika kusafirisha vitu vizito.

An-124 inaweza kubeba hadi tani 150 za mizigo na ina uzito wa kilo 400,000. Umbo lake la ndani lina urefu karibu futi 227 (mita 69.1) na upana wa mabawa ya futi 240 (mita 73.3), ina uwezo wa kusafirisha mizinga, helikopta, na hata ndege nyingine.

Ndege hiyo ina magurudumu mengi ili kutua kwenye njia ambazo hazijatayarishwa vyema. Ndege hiyo imetumika wakati wa operesheni kadhaa za kijeshi na pia inasaidia misheni ya kimataifa ya misaada inapohitajika.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet