Arda Guler kuanza kupata dakika nyingi mwisho wa msimu
Sisti Herman
May 4, 2025
Share :
Akiwa amecheza dakika 1,388 tu kwenye Ligi kuu Hispania tangu msimu uanze, kocha wa Real Madrid amepanga kuanza kumtumia kama mchezaji tegemezi winga wake Arda Guler kwenye mechi za mwisho wa msimu kutokana na jitihada anazozionyesha hivi sasa.
Winga huyo wa timu ya Taifa ya Uturuki hakuwa akipata nafasi ya kuanza mara kwa mara lakini mara nyingi akipata dakika chache amekuwa akizitumia vizuri kulingana na mahitaji ya timu.