Arsenal na Liverpool kwenye vita ya kulipata 'Dole Gumba' la Dean Huijsen
Eric Buyanza
May 14, 2025
Share :
Arsenal na Liverpool zinapambana kumsajili beki wa kati Mhispania kutoka Bournemouth, Dean Huijsen, ambaye pia anawindwa na Real Madrid.
Ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anatamani kujiunga na Real Madrid, vilabu hivi vya Ligi kuu ya Uingereza vyote vimeonyesha vipo tayari kulipa pauni milioni 50 kama ada ya kuachiliwa kwake kama mkataba wake wa sasa unavyotaka.
Ingawa kiasi hicho ni kikubwa, lakini kinaweza kulipwa kwa awamu tatu, ili kurahisisha uhamisho wa mchezaji huyo.