Arteta alipomzidi mbinu Ancelotti, Madrid ikitupwa nje na Arsenal UCL
Sisti Herman
April 17, 2025
Share :
Klabu ya Arsenal jana usiku imeshinda 2-1 dhidi ya Real Madrid kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuiondosha kwenye michuano kwa jumla ya magoli 5-1 baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza kushinda 3-0.
Hii ni tathmini ya mbinu za kocha wa Arsenal Mikel Arteta zilizoweza kuzuia Madrid kufanya ‘Come Back’ kama walivyotarajia.
Kwenye mchezo huo, Mikel Arteta alionekana kuhitaji zaidi kuwa bora kulinda mtaji wa goli 3 aliotoka nao Emirates, hapo tu wangeweza kuvuka hatua hiyo lakini walifanya zaidi kwakufunga magoli
Kwenye lengo kuu la kulinda mtaji wa magoli yake matatu aliyoenda nayo Bernabeu, Arteta alichagua mbinu bora za kuzuia ambazo ziliwafanya Madrid wasiweze kufua dafu kupindua meza
Mbinu za uzuiaji za Arteta Bernabeu zilikuwa nyakati nyingi kuzuia kwa nidhamu kubwa wakiwa wengi nyuma ya mpira na muundo wa 4-4-2 huku wakiweza kuzuia njia za Madrid kwenye theluthi zote tatu za uwanja ambazo walizigawa kwenye nusu mbili.
Kwenye hiyo Moment ya kiuzuiaji wali-dominate na ku-control mechi, Arteta alikuwa na mbinu zenye;
- Muundo wa 4-4-2
- Kuzuia wakiwa pamoja sana, kwenye Blocks zote 3
- Wakichagua nyakati za ku-Press na ku-Block njia za Madrid
Hizi ni mbinu za uzuiaji za Arsenal kwenye nusu mbili za uwanja;
1 . Nusu ya Madrid (High Block)
Madrid wakiwa na mpira kwenye theluthi zao mbili za uwanja hawakuwafuata Madrid kwa Pressure kubwa badala yake walijitahidi kuzuia njia za Madrid ku-Progress Build up zao kwenda mbele kwenye nusu yao huku wakizizuia njia mbili za Madrid, ya kati na pembeni ili kuwalazimisha kupita juu.
(i) Kwenye njia ya kati MERINO na ODEGAARD walizuia mawasiliano ya Asensio, Cortous & Rudigar kwenda kwa viungo wa kati Ferde na Tchoumeni.
(ii) Kwenye njia ya pembeni, SAKA na Martinelli walizuia njia za Asensio, Cortous na Rudigar kwenda kwa Vazquez na Alaba Hapo Arsenal wakawa wamefanikiwa kuzuia Madrid kwenda mbele.
2. Nusu ya pili (Mid & Low Block)
Madrid wakiwa na mpira kwenye theluthi ya kati na nyuma ya Arsenal , au kwenye nusu ya Arsenal, Arsenal walijitahidi kufanya DEPTH ya uzuiaji kuwa ndogo, yaani umbali kutoka mstari wa mbele wa uzuiaji na wa nyuma Nia ni kuwa pamoja na kuzuaji Madrid kucheza katikati ya mistari yao ya uzuiaji
Hapa pia ubora mkubwa wa Arsenal ulikuwa kuwalazimisha Madrid kwenda pembeni na kuzuia Combiantions za pembeni za Madrid mfano;
- Kulia kwa Vazquez, Ferde na Rodrigo
- Kushoto kwa Alaba, Bellingham na Vini
Arsenal walikuwa in numbers na Block ya 4-4-2 Compact
Wakizuia Combinations za pembeni za Madrid, Arsenal walijitahidi kuwa wengi upande huo huku kila mchezaji akiwa na jukumu la kuzuia njia, mfano
- Saka na Timber walijitahidi kuzuia kwenye mapana ya uwanja, Alaba na Vini Jr kuwa huru kupita pembeni upande wa kulia
- Lewis-Skelly na Martinelli walijitahidi kuzuia kwenye mapana ya uwanja, Vazquez naRodrigo kuwa huru kupita pembeni upande wa kushoto
Declan Rice na Partey walijitahidi kuwazuia viungo wa kati wa Madrid, Tchoumeni, Ferde na Bellingham wanaoweza kwenda kutengeneza pembetatu kurahisisha mawasiliano ya wachezaji wa pembeni
Hii ilizuia Combination Play za Madrid katikati ya mistari na kuna nyakati Mbappe alikuwa anashuka hadi chini nje ya BLOCK ya Arsenal kusaidia namna ya kupenya
Kwasababu Strenth kubwa ya Madrid pia huwa ni Side ways Combination, kuna nyakati SAKA na MARTINELLI walilazimika kucheza usawa wa mebeki ili kuzuia Full-Backs wa Madrid wanao-Overlap kutokuwa free na kuwapa situations za 2v1 na Fullbacks wa Arsenal wanao-FOCUS na Vini na Rodrigo
Licha ya kuwa lengo kuu la Arsenal ni kulinda mtaji wa magoli matatu waliyotoka nayo ugenini, lakini pia ulinzi huo uliweza kuwasaidia kupata magoli kwani uzuiaji bora waliweza kupora mipira mipingi na kujibu mashambulizi huku moja likiwa goli la ushindi lililofungwa na Martinelli dakika za jioni
Siyo hivyo tu, Arsenal pia kuna nyakati walikuwa bora kumiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa kuvunja mistari ya uzuiaji ya Madrid, moja kati ya nyakati hizo zilizalisha goli lao la kwanza
Kwa utawala huo wa kila Moment dimbani ni wazi kuwa Arteta alikuwa na mbinu bora zaidi ya Ancelotti Bernabeu.