Aziz Ki aitwa timu ya Taifa akitokea Wydad AC.
Joyce Shedrack
May 22, 2025
Share :
Kiungo Stephane Aziz Ki ameitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Burkina Faso kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya FIFA watakazocheza dhidi ya Tunisia na Zimbabwe.

Katika Orodha ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha Burkina Faso mchezaji huyo ametambulishwa kama mchezaji wa Wydad Athletic na siyo mchezaji wa Yanga.
Nyota huyo ambaye ameonekana akiondoka Nchini siku chache zilizopita bado klabu yake haijaweka wazi kama ni kweli wamemuuza kwenda klabu hiyo ya Morocco na siyo mchezaji wao tena.