pmbet

Baada ya Kikao na Yanga CEO wa Bodi ya Ligi asema mechi ya juni 15 ipo pale pale.

Joyce Shedrack

June 9, 2025
Share :

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo amezungumza baada ya kikao na klabu ya Yanga akiweka wazi kuwa siku ya leo viongozi wa klabu hiyo wamewasilisha mambo manne.

 

"Leo Tulikuwa na Kikao kizuri na Yanga Leo kwenye kikao chetu wenzetu wamekuja na mambo Manne na sisi kama Bodi tuna wajibu wa kuyapokea na Kuyachakata,
 

1. Kuvunjwa Kwa kamati ya uwendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu
2.kujiuzulu Kwa CEO
3.Kujiuzulu Kwa katibu wa Shirikisho la Soka
4.Bodi kuwa Huru
 

Itoshe Kusema Uongozi wa Bodi tumepokea Maazimio Yao na haya yote yapo Nje ya Uwezo wa Bodi isipokuwa Moja tu la kwanza, tumeyapokea haya mengine Matatu na tutayawasilisha Kwa Kamati Tendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu na Mkutano Mkuu wa TFF na Baada ya Hapo Tutawajulisha." Almas Kasongo

 

Aidha,Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi amethibitisha kuwa mchezo namba 184 uliopangwa kuchezwa juni 15 upo pale pale kwa sababu hayo matakwa ya Yanga siyo mchakato wa siku moja.

 

"Mechi ya Juni 15 ipo palepale maana hayo matakwa yao manne sio rahisi kama inavyotajwa, hayo matakwa yao sio mchakato wa siku moja mfano wanataka Bodi ya Ligi iwe huru ijitegemee haiwezi kuwa hivyo kwa siku moja.".

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet