pmbet

Baada ya kushambuliwa na India kwa makombora, Pakistan yasema tutajibu

Eric Buyanza

May 7, 2025
Share :

India imefyetua makombora kadhaa ndani ya ardhi ya Pakistan mapema leo alfajiri na kusababisha vifo vya watu 8, katika mashambulizi yanayoweza kuzusha vita baina ya nchi hizo mbili jirani na hasimu wa miaka mingi. 

Mamlaka za Pakistan zimesema makombora ya India yalililenga jimbo linalozozaniwa na pande hizo mbili la Kashmir pamoja na mkoa wa mashariki wa Punjab. Moja ya makombora liliupiga msikiti kwenye mji wa Bahawalpur na kusababisha kifo cha mtoto mmoja na kujeruhiwa watu wengine kadhaa.

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amelaani mashambulizi hayo ya anga na kusema nchi yake inayo haki ya kulipa kisasi kwa hujuma hizo za India alizozitaja kuwa "kitendo cha kivita".

Mvutano kati ya mataifa hayo mawili umezidi katika siku za karibuni, tangu India ilipoilaumu Pakistan kwa shambulio la wanamgambo lililotokea mwezi uliopita jimboni Kashmir.

India inasema Pakistan inawaunga mkono wale waliotenda tukio hilo lililosababisha vifo vya watu 26.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet