Baada ya miaka 13 mkongwe Modric kuondoka Madrid
Eric Buyanza
May 23, 2025
Share :
Baada ya miaka 13 kiungo mkongwe wa Real Madrid, Luka Modric anatarajiwa kuiaga klabu hiyo baada ya Kombe la Dunia la Vilabu.
Modric mwenye umri wa 39 ameichezea Madrid kwa misimu 13, na kushinda mataji 28 yaliyoweka rekodi kwenye klabu.
"Real Madrid na nahodha wetu Luka Modrić wamekubali kumaliza kipindi kisichosahaulika kama mchezaji wa klabu yetu mwishoni mwa Kombe la Dunia la Vilabu, ambalo timu yetu itacheza kuanzia Juni 18 nchini Marekani," Madrid ilisema katika taarifa Alhamisi.
"Real Madrid ingependa kutoa shukrani zake na mapenzi yake makubwa kwa mtu huyo ambaye tayari ni mmoja wa magwiji wakubwa wa klabu yetu na wa soka duniani.
"Real Madrid inamtakia Luka Modrić na familia yake kila la heri katika hatua hii mpya ya maisha yake. Santiago Bernabéu watampongeza Jumamosi hii kwa ajili ya mechi ya mwisho ya timu yetu ya LaLiga."
"Jumamosi nitacheza mechi yangu ya mwisho Santiago Bernabéu. Nilifika 2012 nikiwa na shauku ya kuvaa jezi ya timu bora zaidi duniani na nikiwa na nia ya kufanya mambo makubwa, lakini sikuweza kufikiria nini kitafuata.
"Kuichezea Real Madrid kulibadilisha maisha yangu kama mchezaji wa soka. Ninajivunia kuwa sehemu ya enzi yenye mafanikio ya klabu bora zaidi katika historia."