Basi jipya la Mwendokasi linalotumia gesi limewasili Tanzania.
Joyce Shedrack
May 9, 2025
Share :
Basi la majaribio la mwendokasi linalotumia gesi lenye uwezo wa kubeba abiria 150 limewasili na litaanza kufanyakazi ndani ya Jiji la Dar es Salaaam.
Basi hilo ni kati ya mabasi 100 yaliyoagizwa na limewasili la kwanza kwa majaribio kisha muuzaji ataendelea kutengeneza mengine 99 kwa kadiri ya mahitaji ya nchi.
Mabasi hayo yanatarijiwa kuhudumia barabara ya Mbezi-Kivukoni na Morocco-Gerezani.