Basi lililowabeba wabunge lapata ajali.
Joyce Shedrack
December 6, 2024
Share :
Basi lililokuwa limewabeba wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliokuwa wakielekea kwenye mashindano ya michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, limepata ajali ya kugongana na lori la mizigo, maeneo ya Mbande, Kongwa asubuhi ya leo, Desemba 6, 2024.
Taarifa iliyoripotiwa kwenye akaunti rasmi za Bunge kwenye mitandao ya kijamii, zimeeleza kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa katika Hospitali ya Uhuru na Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.