Beckham na Gary Neville wanunua Salford United
Sisti Herman
May 13, 2025
Share :
Wachezaji wa zamani wa Manchester United na Uingereza David Beckham na Gary Neville wamekamilisha ununuzi wa klabu ya Salford City, ambayo iko katika ligi daraja la 3 (League Two) ya Uingereza.
Beckham na Neville wamechukua umiliki kutoka kwa wenzao wa zamani wa "Class of '92" wa Manchester United, wakiwemo Paul Scholes, Phil Neville, Nicky Butt, na Ryan Giggs, pamoja na mfanyabiashara wa Singapore, Peter Lim.
Lengo lao ni kuimarisha klabu hiyo na kuifanya iweze kupanda hadi ligi za juu, kama vile Premier League, sawa na mfano wa Wrexham.
Timu hiyo anacheza beki kiraka wa timu ya Taifa ya Tanzania Haji Mnoga.