Beki mwingine kutoka ligi kuu Uingereza kutua Real Madrid.
Joyce Shedrack
May 17, 2025
Share :
Klabu ya Real Madrid imenasa saini ya beki wa kati wa klabu ya AFC Bournemouth na Timu ya Taifa ya Hispania Dean Donny Huijsen kwa mkataba wa miaka mitano hadi mwaka 2030.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 amekamilisha vipimo vya afya usiku wa jana na atajiunga na Real Madrid mapema ili kushiriki michuano ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu mwezi june Nchini Marekani.
Huijsen anakuwa mchezaji wa pili kutoka ligi kuu ya Uingereza ambaye Real Madrid wamefanikiwa kunasa saini zao mpaka sasa baada ya kumalizana naTrent Alexander Arnold.