Benitez aikataa ofa ya Al Ahly
Sisti Herman
May 5, 2025
Share :
Kocha Mkongwe wa Hispania Rafael Benitez ambaye amewahi kuinoa Liverpool, Chelsea, Real Madrid, Napoli na Inter Milan, ameripotiwa kukataa ofa ya kunioa klabu ya Al Ahly ya Misri.
Mashetani Wekundu wa Cairo waliachana na kocha Mkongwe wa Uswizi Marcel Koller wikiendi iliyopita baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na wababe wa Afrika Kusini Mamelodi Sundowns.
Al Ahly walianza mchakato wa kusaka Kocha wa kuchukua nafasi ya Koler haraka na wakawasiliana na Benitez, lakini kocha huyo wa zamani wa Liverpool, Real Madrid, Chelsea, Inter Milan na Newcastle United hakupendezwa na ofa hiyo.
Benitez, ambaye hana kazi tangu alipotimuliwa kutoka kwa klabu ya La Liga Celta Vigo Machi 2024, anaripotiwa kutafuta ofa barani Ulaya na hana hamu ya kwenda Afrika Kaskazini.