pmbet

Benjamin Mkapa Stadium, silaha ya Simba dhidi ya Rs Berkane

Eric Buyanza

April 30, 2025
Share :

Kama kuna silaha ambayo Simba SC wanapaswa kuitumia vyema katika mchezo wao wa Fainali ya CAF dhidi ya RS Berkane ni kiwanja cha Benjamin Mkapa. Hii ni silaha muhimu zaidi katika vita yao na Waarabu wa Morocco.

Jambo zuri ni kusikia siku hiyo ya mchezo huo wa pili wa Fainali uwanja huo uliofungwa utafunguliwa kwa ajili ya mchezo huo. Hii ni miongoni mwa taarifa nzuri kwa Simba SC kuelekea katika mchezo huo. 

Uwanja wa Benjamin Mkapa una makaburi ya timu nyingi. Timu nyingi zimeacha makaburi yao. Hata hawa Berkane kuna kaburi lao pia.

Simba SC anaweza kucheza sehemu nyingine na wakapata matokeo vizuri tu, lakini Simba SC akiwa kwa Mkapa ni kama Simba Mnyama akiwa nyikani katika windo. Anakuwa mtu Mbad.

Ameandika mwanahabari nguli wa michezo wa PMTV @abdulmkeyenge1 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet