Berkane wasilalamike wajikite na suala la kiwanjani
Eric Buyanza
May 23, 2025
Share :
RS Berkane wameingia Tanzania jana jioni kwa Ndege maalum ya kukodi wakitokea kwao Morocco.
Katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar wamewekwa kwa Saa 3 kwa ajili ya taratibu mbalimbali. Wamelalamika na kusema Simba SC imewachezea Faulo katika hili na wako nyuma ya mpango wa wao kuwekwa muda mrefu pale Airport. Ni mshangao na masikitiko. Binafsi nilikuwa na Simba SC katika safari yao ya Morocco.
Pale Airport ya Morocco tulikaa zaidi ya Masaa 4 na hakuna aliyehoji, kulalamika wala kuwataja RS Berkane wako nyuma ya mpango ule. Simba SC ilikamilisha taratibu na tukaondoka pale kwenda zetu Hotelini kupumzika. Berkane wao wana timu bora na wana wachezaji bora, wanaoweza kufanya lolote popte pale, basi wajikite huko katika masuala ya kiwanjani.
Wasitafute Public sympathy kutoka nje na kuanza ambayo hauwezi kuwasaidia katika nyakati hizi. Ukiwa unasafiri na timu za mpira kwenda nje hiki walichokutana nacho Berkane ni kitu cha kawaida. Cha kawaida mno. Nasikia wamegomea kupanda hadi mabasi waliyoandaliwa. Hahahahahaha.
Kila la kkheri Mnyama Simba SC
Amendika mwanahabari nguli wa PMTV @abdulmkeyenge1
Picha kwa hisani ya: Mpekeo Mtandala