Bidii inaweza kumfikisha Lamine kiwango cha Ronaldo na Messi - Flick
Eric Buyanza
May 3, 2025
Share :
Kocha wa Barcelona Hansi Flick amesema jana Lamine Yamal lazima akaze na kuongeza bidii ili aweze kufikia kiwango cha Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
"Sio tu kipaji alichonacho, lakini inahitajika bidii kwelikweli ili aweze kufikia kiwango kama cha Cristiano Ronaldo au Lionel Messi” anasema Hansi.
Simone Inzaghi, kocha wa Inter Milan yeye anasema kipaji alichonacho Yamal mwenye umri wa miaka 17 hutokea kwa nadra sana kila baada ya miaka 50.