pmbet

Bilioni 556,928 zatengwa kukabaliana na Kimbunga Hidaya na Mvua El-nino.

Joyce Shedrack

May 5, 2025
Share :

Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega amesema kwa mwaka 2025/26, pamoja na mambo mengine, Wizara yake itatekeleza miradi mbalimbali ya  matengezo ya dharura za miundombinu ya barabara na madaraja ambayo yaliharibiwa na mvua za El-nino na Kimbunga hidaya Mwishoni mwa mwaka 2023.

Waziri Ulega ameliambia Bunge leo Jumatatu kuwa kupitia programu iliyoidhinishwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya Crisis ans Emergency Responce Component, Jumls ya mikataba 81 yenye thamani ya Shilingi 556,928,617,882.49 kwaajili ya matengenezo ya dharura imesainiwa na makandarasi wanaendelea na kazi maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

 

"Kati ya mikataba hiyo, miradi 72 inatekelezwa na Makandarasi wazawa sawa na Maelekezo ya Mhe. Rais." Amesema Waziri Ulega.

 

Aidha katila hotuba yake ameeleza kuwa katika mwaka ujao wa fedha serikali pia itafanya matengenezo makubwa ya barabara ili zisiendelee kuharibika, ikiwemo bara ara ya Dar Es salaam- Kibiti-Lindi-Mingoyo (Km.463) ambayo ilifungwa kutokana na mvua kubwa zilizonyesha karibuni, akiwahakikishia watumiaji wa barabara hiyo kywa itakapokamilika itakuwa ndiyo suluhu ya changamoto ya kukatika kwa mawasiliano ya mara kwa mara kwenye barabara hiyo nyakati za mvua.

 

Kulingana na Waziri ulega, Makandarasi wawili wa matengenezo ya Barabara ya Mtwara-Mingoyo (Mnazi mmoja)- Masasi kwa gharama ya shilingi bilioni 427 wamepatikana na tayari malipo ya awali yamelipwa na Mkandarasi wa Kipande cha Mtwara-Mingoyo tayari yupo kazini wakati yule wa Mingoyo-Masasi akitarajiwa kuwa uwandani (Site) mwezi huu wa tano, 2025.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet