pmbet

Bill Gates kugawa utajiri wake wa $ Bilioni 200 kwa Afrika

Eric Buyanza

June 3, 2025
Share :

Mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates anasema kuwa sehemu kubwa ya mali yake itatumika kuboresha huduma za afya na elimu barani Afrika katika kipindi cha miaka 20 ijayo.

Akizungumza katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, Tajiri huyo mwenye umri wa miaka 69 aliwataka wavumbuzi wachanga Afrika kufikiria jinsi ya kuimarisha teknolojia ya Akili Mnemba (AI) ili kuboresha huduma za afya katika bara hilo.

Mwezi uliopita Gates alitangaza kwamba atatoa 99% ya utajiri wake mkubwa - ambao anatarajia utafikia $200bn (£150bn) - ifikapo 2045, wakati ambapo taasisi yake itakamilisha shughuli zake.

"Hivi majuzi nilitoa ahadi kwamba utajiri wangu utatolewa katika kipindi cha miaka 20 ijayo.

Sehemu kubwa ya ufadhili huo itatumika kukusaidia kutatua changamoto hapa Afrika," alisema katika hotuba yake katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU).

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet