pmbet

Billnass atoa ushauri mzito kwa vijana akiri umaarufu umejaa ushetani.

Joyce Shedrack

June 11, 2025
Share :

Staa wa muziki wa Bongo Fleva na mume wa mmiliki wa lebo ya The African Princess, Billnass ametoa ushauri kwa vijana ambao wanavipaji vinavyohusisha umaarufu huku akiwataka kuwa wavumilivu kwani tasnia nyingi zimejaa mambo mengi mabaya.

Kupitia Insta story ya ukurasa wake Instagram Billnass ameandika ujumbe huo mzito akisisitiza kuwa kwenye umaarufu kuna kila aina ya vita,usaliti,ushetani na dhuluma.

"To all Young People, Wadogo zangu na rafiki zangu miliobarikiwa vipaji mbalimbali, Kabla ya kuingia kwenye tasnia yoyote inayohusiana na umaarufu Tanzania!! Muombe sana Mungu akupe nguvu ya uvumilivu na Roho ya kustahimili!! huku kuna kila aina ya vita, Usaliti, Ushetani, Dhuruma kuanzia kwa wadau, Managers, Distribution Company, Labels”. 
 

“Swala la kutajilika au kupata pesa kupitia hizi kazi sio rahisi kama unavosikia ila kupata msongo wa mawazo, kupoteza maisha, kupata maradhi, kuchanganyikiwa ama kuingia kwenye Addiction mbalimbali ni rahisi kuliko kutengeneza pesa, ni vyema kuwa na umakini sana na kuingia kwenye tasnia ukiwa na utayari lakini usiache kumuweka Mungu kwanza.

Maana unaweza kupambana ili uisaidie familia yako kumbe unaenda kuleta janga ambalo familia yako ndo itakuwa kwenye jukumu la kuteseka kukusaidia" Ameandika Billnass.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet