Binti wa Rais aliyejiunga na mgambo ili kupambana na ujangili
Eric Buyanza
July 24, 2025
Share :
Tariro Mnangagwa ni Binti wa Rais wa Zimbabwe Amerson Mnangagwa. Binti huyu aliyezaliwa mwaka 1998, amejikita zaidi katika sekta ya filamu akiwa mtayarishaji wa filamu na muigizaji.
Tariro amesifika kwa utayarishaji wa filamu kama vile Gonarezhou na Nehanda, akiigiza pia katika filamu zote mbili.
Yeye ndiye binti mdogo wa rais wa sasa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa na mkewe wa kwanza Jayne Matarise, ambaye alifariki mwaka 2002 kwa saratani ya shingo ya kizazi.
Binti huyu alipata Diploma ya upigaji picha huko Cape Town nchini Afrika Kusini.
Pia alihitimu shahada ya Usimamizi wa Michezo katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Cape Peninsula.
Baada ya kurejea Zimbabwe, Tariro alijiunga na 'Akashinga', kitengo cha mgambo wa kupambana na uwindaji haramu. Kisha akawa mwanachama wa kitengo cha kupambana na uwindaji haramu cha wanawake.
Tariro, amejiunga na kundi la walinzi vijana waliojitolea kupambana na ujangili katika bonde la Zambezi.
Takriban wanawake 36 wanaunda kitengo cha kupambana na ujangili ambacho kinafundishwa na kitengo cha walinzi wa uwanja cha Akashinga cha International Anti-Poaching Foundation kukabiliana na majangili katika eneo hilo.
BBC