Birthday ya CCM kufanyika Dodoma.
Joyce Shedrack
January 29, 2025
Share :
Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 48 ya Kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) inatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri, February 05.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo atakuwa Mwenyekiti wa CCM na Mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hivi karibuni watu mbalimbali pamoja na viongozi wa CCM walikuwa jijini humo katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM.
Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo ya kufikisha Miaka 48 ni UMOJA WETU; NGUVU YETU.