pmbet

Bora nimuweke benchi kocha wa Makipa siyo Marcus Rashford.

Joyce Shedrack

January 27, 2025
Share :

Kocha Mkuu wa klabu ya Manchester United Ruben Amorim amesema bora ampe nafasi ya kucheza kocha wa Magolikipa wa Manchester United mwenye umri miaka 63  Jorge Vital badala ya kumtumia mchezaji ambaye hajitumi kama Marcus Rashford.

Marcus Rashford: Ruben Amorim suggests he'd rather pick 63-year-old coach  over forward - BBC Sport

Amorim ameyasema hayo wakati alipoulizwa swali baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Fulham siku ya jana huku akiweka wazi kama mambo hayatabadilika na yeye pia hatabadilika.

"Sababu za kutomchezesha mshambuliaji huyo ni zile zile haoneshi ari wakati wa mazoezi pamoja na mtindo wake wa maisha ya kila siku, Kama mambo hayatabadilika, nami sitabadilika hali ni sawa kwa kila mchezaji ukijitahidi na kufanya mambo sahihi, tunaweza kukupa nafasi katika kikosi."

"Unaweza kuona kwamba tunakosa mchezaji mwenye kasi kwenye benchi, lakini bora kumchezesha kocha wa makipa, Jorge Vital, uwanjani badala ya kumtumia mchezaji ambaye hajitolei kwa uwezo wake wote." amesema Amorim.

Rashford ametimiza wiki sita pasipo kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha Manchester United huku kukiwa na tetesi kwamba huwenda akaondoka kwa mkopo kabla ya dirisha dogo la uhamisho kufungwa akihusishwa kutimkia Bayern Munich au Barcelona.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet