Bosi Simba aendelea 'kumkaba Kooni' Camara
Joyce Shedrack
October 20, 2024
Share :

Baada ya kupoteza 1-0 kwa wapinzani wao Yanga kwenye mchezo wa jana wa dabi ya Kariakoo, mmoja ya wajumbe wa Bodi ya Simba Crescentius Magori ameendelea kumnyooshea kidole kipa wao Moussa Camara katika kosa alilofanya likazaa bao la ushindi dhidi ya Yanga leo katika mchezo wa Derby Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Mkapa.
Kupitia mtandao wa Instagram, Magori amemwita mara tatu Mlinda mlango huyo na kumwambia hata kwao Conakry watafika.
Baada ya chapisho hilo Magori asubuhi ya leo amechapisha tena kuwa hakukosea kuandika vile bali alikuwa sahihi kwa kusudi lake na ataongea leo.





