pmbet

Brazil ilihitaji kocha wa 'Jina Kubwa' kama Ancelotti - Casemiro

Eric Buyanza

May 16, 2025
Share :

Kiungo wa kati wa Manchester United Casemiro amepongeza kuajiriwa kwa Carlo Ancelotti kuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil, akisema kuwa nchi yake "ilihitaji" kocha maarufu kama huyo.

Casemiro alishinda mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa na taji la LaLiga katika misimu yake mitatu aliyocheza chini ya Ancelotti huko Madrid.

“Baada ya Tite kuondoka nadhani ilibidi awe yeye, Casemiro aliiambia ESPN, Brazil ilihitaji mtaalamu kama yeye, Brazil ilihitaji jina kubwa kama yeye, mtu ambaye anaheshimika."

Adenor Leonardo Bacchi, maarufu kama 'Tite' mwenye umri miaka 63 kwa sasa ndiye aliyekuwa kocha wa Brazil kuanzia mwaka 2016 hadi 2022.

"Huyu jamaa ni wa kipekee kwa jinsi anavyozungumza kuhusu soka na jinsi anavyolielewa soka, wacha tufurahie bila kujali kama atashinda au atashindwa kwa sababu huyu mtu anapozungumza juu ya mpira wa miguu, ana haiba na nguvu ya kuwafanya wachezaji wafanye vizuri"

"Nina furaha kwamba kocha wa hadhi kama hii anafundisha timu ya taifa ya Brazil" alimalizia Casemiro.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet