Bunge la Ulaya kujadili sakata la Lissu Kesho
Sisti Herman
May 6, 2025
Share :
Bunge la Ulaya linatarajiwa kukutana kesho Mei 7, 2025 kwa kikao cha dharura kujadili suala la Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu.
Lissu, ambaye anakabiliwa na kesi mbili ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni na ya uhaini kosa ambalo akitiwa hatiani adhabu yake ni kifo.
Kwa sasa kesi hizo zinasikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Wakati Lissu akiwa mahabusu akikabiliwa na mashitaka hayo, Chadema ambayo iligomea kusaini Kanuni za Uchaguzi, na kwa kushindwa kufanya hivyo kimekosa fursa ya kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2025 kwa mujibu wa sheria za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Mjadala wa Bunge la Ulaya utafanyika chini ya mwavuli wa kujadili hali ya kile wanachokiita ‘haki za msingi, haki za binadamu na demokrasia kwa ujumla.’
Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Bunge hilo, mjadala huo utaanza saa 7:00 mchana hadi saa 4:00 usiku kwa saa za Ulaya.
Baada ya majadiliano hayo kutatolewa azimio linalojulikana kama "2025/2690 (RSP)" na wabunge wa Bunge la Ulaya watapiga kura kuhusu azimio hilo Mei 8, 2025.