Bunge la Ulaya lashinikiza Lissu kuachiwa huru
Sisti Herman
May 8, 2025
Share :
Bunge la Ulaya limetoa maazimio sita kwa Tanzania ikiwamo kutaka haki na kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,Tundu Lissu.
Aidha,linaitaka Serikali ya Tanzania kumuachilia mara moja na bila masharti, kumhakikishia usalama wake, haki ya kesi na uwakilishi wa kisheria;
Aidha, linaitaka Serikali ya Tanzania kuirudishia CHADEMA haki yake kamili ya kushiriki katika uchaguzi wa Oktoba 2025.
Pia linaitaka EU na Nchi wanachama wake kufuatilia kwa karibu mamlaka za Tanzania kuhusu kesi ya Lissu na kufuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hiyo.