Burna Boy kufanya shoo ya bure Burkina Faso.
Joyce Shedrack
May 19, 2025
Share :
Mkali wa muziki wa Afrobeat kutoka nchini Nigeria Burna Boy amefunguka kuwa anatamani kufanya shoo ya bure Burkina Faso mwishoni mwa mwaka huu.
Burna ameweka wazi matamanio hayo kupitia ukurasa wa Instagram wa No Sign Of Weakness Tv 'nsw.tv' ambao ni ukurasa rasmi wa kutangaza albamu yake inayotarajiwa kutoka kati ya Mei au Juni mwaka huu.
Burna amesema kama itawezekana atafurahia kuwapa watu wa Burkina Faso burudani ya bure kabla ya mwaka huu kuisha.
"Kama itawezekana itakuwa jambo la heshima kuwapa watu wa Burkina Faso shoo ya bure muda fulani mwaka huu kabla ya kumalizika Inshaallah," ameandika.
Burna Boy hutoza dola 1 milioni zaidi ya sh2 bilioni kwa onyesho moja lakini endapo onesho hilo litafanyika pesa zitakazopatikana zitatolewa kwa Rais Ibrahim Traore ili kusaidia katika shughuli za kuendeleza nchi hiyo.