Cardi B amuweka hadharani mpenzi wake mpya
Eric Buyanza
June 3, 2025
Share :

Mwanamuziki wa Marekani Cardi B amemtambulisha rasmi Stefon Diggs kama mpenzi wake mpya, Diggs ni mchezaji wa mchezo maarufu nchini Marekani wa (American Football).
Cardi B alifanya hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumatatu (jana) kwa kuchapisha picha kadhaa za kimahaba kuthibitisha mahusiano yao.
Haya yanajiri katikati ya drama ya talaka inayoendelea kati ya Cardi B na aliyekuwa mume wake Offset.
Agosti 2024 Cardi B aliwasilisha kesi ya talaka kufuatia wawili wao kuwa na tofauti zisizoweza kusuluhishwa.





