pmbet

Cassie Ventura azua gumzo kwa ushahidi alioutoa kesi ya Diddy.

Joyce Shedrack

May 14, 2025
Share :

Aliyewahi kuwa mpenzi na msanii wa lebo ya Rapa wa Marekani Sean Diddy Combs mrembo Casandra “Cassie” Ventura siku ya jana alitoa ushahidi mahakamani dhidi ya kesi zinazomkabili Diddy huku akieleza jinsi alivyoteseka kisaikolojia na kimwili kwa miaka 11.

Watching her have sex with other men, physical abuse: Most shocking  revelations by Sean 'Diddy' Combs' ex Cassie Ventura - Hindustan Times
Cassie alieleza jinsi alivyoanza mahusiano na Diddy ambapo alieleza kuwa walikutana wakati yeye akiwa na umri wa miaka 19 na kipindi hicho Diddy alikuwa na miaka 38 na kusaini mkataba wa kutoa albamu 10 chini ya lebo yake ya ‘Bad Boy Records’ lakini alifanikiwa kutoa albamu moja pekee.
 

Msanii huyo aliweka wazi kuwa alivutiwa na Diddy kutokana na ucheshi wake na alianza kushiriki naye mapenzi wakati alipofikisha miaka 22 na ndipo alianza kunyanyaswa kingono na msanii huyo.

Katika maelezo yake Cassie ameeleza kuwa Diddy alimshirikisha namna anavyofurahia kuwatazama wengine wakifanya tendo la ndoa na akaamua kufanya kitendo hiko na wanaume wengine ili kumridhisha mpenzi wake.

Mwanadada huyo amefunguka zaidi kuwa Diddy alianza kupanga vitendo hivyo ambavyo vilihusisha kuajiri wanaume wengine kufanya nao mapenzi na kupanga vyumba vya hoteli kwa ajili ya kufanya matukio kama hayo mara kwa mara.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet