pmbet

CCM itashinda kutokana na kazi nzuri za Rais Dkt.Samia.

Joyce Shedrack

May 8, 2025
Share :

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo (CCM),CPA Amos Makallla amewaomba wananchi wa  jimbo la Mikumi kukiunga mkono chama hicho, katika uchaguzi mkuu .

 

CPA Makalla ametoa kauli hiyo leo Alhamisi wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Ruaha Jimbo la Mikumi wilayani Kilosa aliposimama kuwasalimia akielekea Kilombero.

 

Makalla amesema hapo zamani wananchi wa Morogoro katika majimbo ya Kilombero, Mikumi na Mlimba walionjeshwa sumu, lakini hivi sasa waliowaonjesha( Chadema) hawatashiriki tena.

 

Kutokana na hilo, CPA Makalla amewataka wananchi wa Morogoro kwa kujiandikisha ili kupata fursa ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ili kukiwezesha cham hicho kupTa ushindi mnono.

 

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoshiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu ni  mserereko wa ushindi kwa chama hicho tawala.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet