CCM yawabaini wanaohonga wajumbe kupewa Ubunge Shinyanga
Sisti Herman
May 11, 2025
Share :
Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama kimesema, watia nia 9 wa nafasi za Ubunge na Udiwani wilayani humo, wamebainika kujihusisha na vitendo vya kugawa fedha kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM nyakati za usiku, kinyume na maadili ya Chama
Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Chatwanga, amesema Wagombea hao wanatoka kwenye Majimbo yote matatu ya Wilaya hiyo: Kahama Mjini (5), Ushetu (2) na Msalala (2)
Ameeleza “Tumebaini baadhi ya watia nia wanazunguka usiku kwenye Kata mbalimbali kuwapa Wajumbe Fedha, wengine hadi Tsh. 10,000 ili wawapitishe kwenye mchakato wa ndani. Hii ni aibu, ni udhalilishaji na ni kinyume cha Maadili ya CCM. Chama hakiwezi kumvumilia Mgombea wa aina hiyo."