pmbet

CHAUMMA yapokea wanachama elfu tatu wa kutoka CHADEMA.

Joyce Shedrack

May 21, 2025
Share :

Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimewapokea wanachama wapya zaidi ya 3,000 waliotoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo baadhi ya waliokuwa viongozi wa chama hicho.

Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Hashim Rungwe wakati wa hotuba ya kuwapokea maelfu ya wanachama wapya iliyofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam amesema siku ya leo ni siku muhimu katika historia ya Chama hicho.

 

Leo ni siku ambayo tunaandika historia mpya ya chama chetu (Chama cha Ukombozi wa Umma) tangu kilipopata usajili wa kudumu mwaka 2012, ni takribani miaka 13 sasa tumeendelea na safari ya kujenga chama chetu hatua kwa hatua katika mapito mbalimbali na hatimaye tumefikikia siku hii muhimu katika historia yetu kama chama na Taifa kwa ujumla" -Rungwe

"Tunakumbuka kuwa waasisi wa Taifa letu (Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume) walikuwa na makusudi walipopigania uhuru wa Taifa letu walikuwa na ndoto kuhusu jamii ambayo waliitaka kuijenga, walikusudia kujenga jamii ambayo pamoja na tofauti lakini jamii yenye usawa katika mahitaji ya msingi na lazima" -Rungwe

"Walikusudia kujenga jamii ambayo watu watashindana katika ziada lakini lakini wote wanakuwa sawa katika kupata mahitaji ya msingi ya heshima na utu wao" -Rungwe.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet