Che Malone awatisha Waarabu tumekuja kushinda fainali hatujaja kucheza.
Joyce Shedrack
May 16, 2025
Share :
Mchezaji wa klabu ya Simba Che Malone Fondoh ameonekana kuwa na ujasiri mkubwa kuelekea mchezo wa kesho wa fainali Nchini Morocco akisema wameenda Nchini humo kushinda mchezo wa fainali na siyo kucheza.
Akizungumza na waandishi wa habari katika dimba la Manispaa ya Berkane beki huyo amesema"Kutinga fainali tunawajibika kucheza na kushinda tupo hapa kushinda mchezo wa fainali hatupo hapa kucheza fainali" .
Mnyama atacheza mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya RS Berkane.
Mechi hiyo itapigwa Mei 17, 2025, saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania, ambapo hapa Morocco itakuwa saa 2:00 usiku.