pmbet

Chelsea yakamilisha usajili wa wachezaji wawili kwa Bilioni 220

Eric Buyanza

March 20, 2025
Share :

Chelsea imekamilisha usajili wa wachezaji wawili wa Sporting viungo Geovany Quenda na Dario Essugo kwa dau la jumla ya takriban £62.4m, klabu hiyo ya Ureno imesema. 

Winga Quenda, 17, atajiunga na Chelsea kwa ada ya hadi £44m kulingana na tangazo kwenye tovuti ya Sporting, lakini atasalia Lisbon hadi mwisho wa msimu wa 2025-26. 

Kinda huyo ameingia kwenye kikosi cha kwanza cha Sporting msimu huu na kucheza Ligi ya Mabingwa mwezi Septemba. 

Essugo, kiungo mkabaji mwenye umri wa miaka 20, atahamia Stamford Bridge msimu wa joto baada ya kucheza kwa mkopo Las Palmas. 

Sporting ilitangaza ada yake ya uhamisho kuwa £18.4m. Amefanya vizuri nchini Uhispania, lakini pia amepata kadi nyekundu mbili katika mechi zake nne zilizopita. 

Wakati mashabiki wa Chelsea wakilazimika kusubiri kwa muda kumuona Quenda, Essugo anaweza kuungana na kikosi cha Enzo Maresca kwa ajili ya Kombe la Dunia la Klabu ya Fifa msimu huu wa kiangazi nchini Marekani. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet