pmbet

Chemical atunukiwa shahada ya uvamivu 'PHD' Uingereza.

Joyce Shedrack

April 30, 2025
Share :

Rapa Maarufu wa kike Nchini Claudia Lubao maarafu kama Chemical ambaye alikuwa masomoni Uingereza ametunukiwa shahada ya Uzamivu (PhD) na chuo cha St. Andrews nchini humo.

Chemical amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa instagram akiweka wazi kuwa kufikia hatua hiyo ya elimu ilikuwa ni moja ya ndoto yake ambayo kwa sasa imetimia.

"Niliwahi kuwa na ndoto na leo nimeamka kama Dk Lubao. Nina shauku zaidi ya kushiriki kwamba nimepitisha rasmi PhD Viva yangu, ninaheshimu na kushukuru sana kwa usaidizi wa ajabu ambao nimepata kutoka kwa wasimamizi wangu, idara shirikishi, kamati ya ukaguzi, wasahihishaji, washiriki.

"Wafanyakazi wenzangu, marafiki, muziki na familia yangu, na kila mtu ambaye alinitia moyo katika safari hii yote ya kuwa Dk. Lubao.
Usiku usio na usingizi, kujitolea, uvumilivu yote yamelipa," ameeleza Chemical.

Utakumbuka, Chemical aliwahi kutunukiwa tuzo kutoka University Of Dar es Salaam mwaka 2021, kwa kuwa mwanafunzi mwenye tafiti bora zaidi 2020/2021 ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika;

"Nimekua mwanafunzi mwenye tafiti bora (first winner) kwa chuo kizima kwa mwaka 2020/21. Chuo cha UDSM ni kikubwa wanafunzi ni wengi na wanafanya vitu vikubwa sana.Mimi kushinda nafasi hii ilikua ni ndoto ambayo sikuwahi kuiota.

"Lakini namshukuru mwalimu wangu Dr. Elgidius Ichumbaki kwa kusimamia taaluma yangu, kuni-train mpaka leo niliyohisi hayawezekani yamewezekana thank you team for mentoring me. Niseme tu kwamba miaka miwili niliyotulia kwenye muziki haikwenda bure," ameandika Chemical.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet