Davido Am-surprise mke wake na zawadi ya gari la kifahari G-WAGON G63 ya mwaka huu.
Joyce Shedrack
May 1, 2025
Share :
Staa wa muziki wa Nigeria David Adeleke maarufu Davido amemfanyia 'Surprise' mke wake Chioma kwa kumzawadia gari jipya la kifahari aina ya G Wagon G63 ya mwaka 2025 kama zawadi ya kufikisha miaka 30 wakiwa huko Atlanta nchini Marekani.

Wawili hao ambao wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa takribani miaka nane walifunga ndoa ya kifahari mwezi june mwaka jana na mpaka sasa wana watoto wawili pamoja wakike na wakiume ambao ni mapacha waliofanikiwa kuwapata mwaka 2023.