Diamond Platnumz awagaragaza vibaya wasanii wa Nigeria aweka rekodi Afrika.
Joyce Shedrack
May 6, 2025
Share :
Staa wa Bongo Fleva nchini Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza ukanda wa jangwa la Sahara kufikisha ‘Subscribers’ milioni 10 kwenye mtandao wa Youtube.
Diamond alifungua rasmi ukurasa huo wa Youtube Juni 12, 2011 na mpaka sasa ana zaidi ya watazamaji zaidi ya bilioni mbili kutoka kwenye video 1,075 alizopandisha katika mtandao huo huku akiweka rekodi hiyo ya kuwa na Subscribers milioni 10.
Mmiliki huyo wa lebo ya WCB anawizidi wasanii wakubwa wa Afrika wakiwemo wa Nigeria kama Rema, Davido, Asake, Harmonize, Rayvanny, Wizkid na wengine wengi.
Hii si mara ya kwanza Diamond kuwa na namba za kushangaza na kuwaacha mbali mastaa wengine wa Afrika kwani mwaka 2020 alitajwa kama msanii ambaye anaongoza kuwa na watazamaji wengi Afrika kupitia mtandao huo alipoweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kufikisha watazamaji bilioni 1 kwenye mtandao huo.