Diamond Platnumz na Davido kwenye birthday party ya Bilionea wa Ghana.
Joyce Shedrack
March 21, 2025
Share :
Staa wa muziki wa bongofleva @diamondplatnumz pamoja na wanamamuziki wakubwa Afrika akiwemo David Adeleke maarufu @davido na wengine kama @stonebwoy @kidimusic wanatarajia kusimamisha Jiji la Accra Ghana Kwenye Sherehe za Kumbukizi ya Kuzaliwa kwa Bilionea wa Nchi hiyo Richard Quaye.

Sharehe hizo zinazoanza Siku ya Leo March 21 Zinatarajia kufunga jiji la Accra, na kuwa na Mfululizo wa Bata za Usiku , Vyakula Vya Kila aina, na Burudani za Viwango Vya Juu .
Bilionea huyo anataka kufanya Sherehe hizo kuwa ni Tukio litakalozungumziwa Zaidi Barani Afrika kwa Mwaka Huu na tayari Mkurugenzi wa lebo ya WCB Wasafi Diamond Platnumz ameondoka Nchini kwenda kwenye sherehe hiyo.





